BurudaniHabari

Mpenzi wa zamani wa Tiger Woods adai kulipwa Tsh bilioni 70 kwa kufukuzwa nyumbani

Kesi iliyowasilishwa na mpenzi wa zamani wa Tiger Woods inadai kwamba alimdanganya kubeba begi na kuondoka katika nyumba yao ya pamoja kabla ya kumfungia nje.

Mawakili wa Erica Herman, ambaye alianza kuchumbiana na mchezaji huyo wa gofu mwaka wa 2017, wanahoji anahitaji kulipwa $30m (£25m) sawa na T sh 70,200,000,000/= kutokana na jinsi alivyofukuzwa ghafla kutoka kwa nyumba hiyo.

Katika kesi nyingine, anataka makubaliano ya kutofichua (NDA) aliyotia saini na Bw Woods kufutiliwa mbali

Mwakilishi wa Bw Woods, 47, hakutoa maoni yake mara moja.

Kutengana kwa wanandoa hao hakujatangazwa rasmi. Hawajaonekana pamoja hadharani tangu kuhudhuria mashindano ya tenisi ya US Open huko New York Agosti mwaka jana.

Bi Herman, 38, aliwahi kufanya kazi katika mgahawa wa bingwa huyo mara 15 wa Florida, The Woods Jupiter.

Kesi aliyofungua Oktoba dhidi ya wakfu wa nyumba inayoshikiliwa na Bw Woods ndiyo imeibuka sasa. Inadai kuwa alifungiwa nje ya nyumba yao ya pamoja huko Hobe Sound, Florida.

“Hasa, kwa hila, maajenti wa mshtakiwa walimshawishi mshtakiwa kubeba koti kwa ajili ya likizo fupi na, alipofika uwanja wa ndege, walimwambia kuwa alikuwa amefungiwa nje ya makazi yake,” kulingana na hati za mahakama zilizoonekana.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents