Mpiga gitaa maarufu wa Kongo aliyefanya kazi na Kanda Bongo Man, Lokassa Ya M’Bongo amefariki Dunia akiwa na umri wa miaka 76, msaidizi wake wa karibu Ngouma Lokito amethibitisha.
Lokassa Ya M’Bongo amekuwa akisumbuliwa na maradhi ya moyo kwa muda mrefu kabla ya umauti kumfika usiku wa Machi 15, 2023 akiwa Nashua, New Hampshire nchini Marekani.
Imeandikwa na @fumo255