Habari

Mpina ashinda kesi, kurudi ulingoni kuwania urais

Mgombea Urais wa Tanzania kupitia ACT-Wazalendo, Luhaga Mpina leo Septemba 11, 2025 ameshinda kesi ya kupinga kuzuiwa kurejesha fomu za uteuzi wa mgombea Urais iliyofunguliwa dhidi ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, na mahakama kuamuru taratibu ziendelee zilipoishia.

Katika uamuzi uliotolewa Agosti 26, 2025 na Msajili wa Vyama vya siasa alibainisha kuwa Mpina hakutimiza vigezo vya uanachama kwa mujibu wa kanuni za chama, akisema kuwa alijiunga ACT-Wazalendo nje ya muda uliopangwa na hivyo hakustahili kuwania nafasi ya urais kupitia chama hicho.

Uamuzi huo umetolewa leo wakati kesi hiyo iliposikilizwa na hatimaye Mpina kupata ushindi hivyo anatarajiwa kurejesha fomu ya kuteuliwa kugombea urais kupitia Chama cha Act Wazalendo

Written by Janeth Jovin

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents