Habari

Mradi wa uwekezaji wa wasichana na wanawake vijana washinda tuzo

Mpango wa Tigo wa Uwajibikaji kwa Jamii kwa kushirikiana na Apps and Girls, shirika lisilo la kiserikali nchini limeibuka mshindi kama mabingwa watano bora wa 2023 WSIS PRIZE duniani chini ya kitengo cha E-employment na kushinda washindani wengine 109 kutoka duniani kote.

Mpango wa Jovia chini ya mradi wa Kuwawezesha Wasichana na Vijana wa Kike ulitambuliwa kwa kushughulikia mgawanyiko wa kijinsia wa kidijitali kwa kutoa mafunzo ya TEHAMA & Ujasiriamali na kulea wasichana na wanawake vijana chipukizi wasiojiweza nchini Tanzania.

Mshindi wa jumla wa 2023 WSIS PRIZES alitangazwa na kutunukiwa tuzo siku ya Jumanne tarehe 14 Machi 2023 huko Geneva Uswisi wakati wa Jukwaa la WSIS la 2023 lililoandaliwa na ITU (Umoja wa Kimataifa wa Mawasiliano) UNESCO, UNDP na UNCTAD, kwa ushirikiano wa karibu na WSIS Action Line, wawezeshaji na mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa. Ukweli kwamba mpango wa Uwezeshaji Wasichana na Vijana wa Kike ulishinda miongoni mwa miradi bora ya TEHAMA ya WSIS, unaonyesha lengo la Tigo la kumwezesha mtoto wa kike kwa kutoa fursa ya kujumuishwa zaidi kidijitali nchini Tanzania.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents