Habari

Mramba aipongeza EWURA kwa huduma wanazozitoa

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba ameipongeza Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati (EWURA) kwa huduma nzuri ambayo wamekuwa wakiifanya na kwamba kama wizara watahakikisha mamlaka hiyo inafanyakazi yake kulingana na sheria pamoja na sera zilizowekwa.

Mramba ameyabainisha hayo alipotembelea katika Banda la EWURA lililopo kwenye Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa(DITF) maarufu kama Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es salaam.

Amesema wizara hiyo itaendelea kuisaidia Ewura ili iweze kutekeleza majukumu yake katika Mazingira wezeshi.

“Ewura inafanya kazi nzuri mpaka sasa hivi, kama mnavyoona huduma zinazodhibitiwa na mamlaka hii zinapatikana na wameweza kudhibiti Upatikanaji wa huduma yenyewe ya nishati, bei inayotolewa na ubora wa huduma hiyo.

“Kwenye eneo la bei nafikiri mnafahamu kuwa nchi yetu ni miongoni mwa nchi zenye bei ya chini sana ya huduma za umeme. Lakini Kwa siku za hivi karibuni tumeshuhudia kuwa bei ya umeme zimezidi kuimarika, kule kukatika kwa umeme mara Kwa mara kumepungua,” amesema na kuongeza kuwa:

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Dk. James Mwainyekule, amesema mwezi uliopita walisaini mkataba na Tanesco kupima utendaji kazi na namna ya utekelezaji kazi.

“Uwekezaji huu unafanywa na serikali ambapo hadi Juni 30, mwaka huu ubora wa mafuta ulifikia asilimia 97. Tunazingati bei katika soko la dunia tukifuatilia na kila mwezi bei zilishuka na kupanda kulingana na soko la dunia.

“Magari takribani 5,000 yanatumia gesi hadi sasa na hii imesaidia kwa asilimia kubwa kupunguza dola kutumika katika kiagiza mafuta nje, kwa sababu gesi hii ya mafuta inatoka nchini.”

Written by Janeth Jovin

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents