Tragedy

Mrembo ajiua kwa kujirusha ghorofani kisa Likes 10k za mtandao wa Instagram

Msichana mmoja nchini Malaysia anayekadiriwa kuwa na miaka 16 amejiua kwa kujirusha kutoka ghorofa ya 3 kwa kile kilichoelezwa kuwa ni msongo wa mawazo uliotokana na mtandao wa Instagram.

Related image

Kwa mujibu wa Polisi mjini Kuching, wamesema tukio hilo limetokea jana katika kisiwa cha Borneo ambapo wamedai kuwa masaa mawili yaliyopita aliweka posti kwenye ukurasa wake wa Instagram na kuandika “Ni jambo muhimu sana kwangu, Nataka kujua wangapi wanataka nife na wangapi wanataka niendelee kuishi“.

Kisha akaweka Hashtag ya Wanaotaka nife nahitaji Likes 10k na kama hutaki Komenti, baada ya masaa mawili ikatolewa taarifa amejirusha ghorofani.

Tutaendelea kufanya uchunguzi zaidi kwani hizo ndio taarifa za awali, na wakati anafanya hivyo alikuwa peke yake chumbani ni binti wa miaka 16 (Jina limehifadhiwa) na wazazi wameeleza kuwa alikuwa na matatizo chuoni kwake,“amesema Aidil Bolhassan mkuu wa Jeshi la Polisi Mjini Kuchin.

Chanzo: Daily Mail

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents