Siasa

Mrithi wa Maalim Seif alivyoapishwa leo Ikulu Zanzibar (+ Video)

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Othman Masoud ameapishwa rasmi leo kuchukua wadhifa huo mpya baada ya kifo cha mtangulizi wake Maalim Seif.

Hafla ya kuapishwa kwake imefanyika katika Ikulu ya Zanzibar saa nne kwa saa za Afrika ya Mashariki, tukio lililotangazwa moja kwa moja kwenye televisheni.

Baada ya kutangazwa kwa uteuzi wake hapa jana Bw Othman Masoud alisema hakuna anayeweza kukidhi vigezo wala viwango vya mtangulizi wake Maaalim Seif. Hakuna na hatotokea, alisema.

‘’Najua shauku na hamasa zenu kwa maendeleo ya nchi yetu. Najua imani yenu kwangu, hata wale waliokuwa wakihoji juu ya uwezo wangu au kufaa kwangu kwa nafasi hii walifanya hivyo kwa nia safi na hamu ya kupata mtu atayekidhi haja’’,imesema taarifa ya hotuba yake baada ya uteuzi.

Bw Masoud anaapishwa rasmi hii leo kuchukua wadhifa huo mpya baada ya kifo cha mtangulizi wake Maalim Seif.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents