Habari
Msajili vyama vya siasa akutana na viongozi wa Chadema
Na Janeth Jovin
Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini Jaji Francis Mutungi amekutana na viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa lengo la kujadili ili kuimarisha demokrasia nchini.
Imeelezwa kuwa kikao cha Msajili na Chadema kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam ni juhudi za ofisi hiyo kuimarisha hali ya kisiasa hususan demokrasia ya vyama vingi vya siasa nchini.
Miongoni mwa viongozi waandamizi wa Chadema ni Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe na Katibu Mkuu Chadema John Mnyika.