Habari

Msako mkali kwa wanaharakati wa kundi la ‘Last Generation’

Polisi ya Ujerumani imefanya Misako katika nyumba za wanaharakati kadhaa, wa kundi lujulikanalo kama ‘Last Generation’ yaani Kizazi cha Mwisho, ikiwatuhumu kuunga mkono kile walichokitaja kuwa “chama cha uhalifu”.

Mkuu wa mashtaka wa wilaya ya Neuruppin katika jimbo la Brandenburg ameliambia shirika la habari la AFP kwamba, misako hiyo imefanywa katika maeneo 11 kote Ujerumani.

Uchunguzi dhidi ya wanaharakati hao umechochewa na maandamano yao ya mwezi Aprili walipofunga mabomba ya nishati na mafuta hivyo kuathiri maeneo kadhaa ikiwemo kiwanda cha mafuta cha PCK katika mji wa Schwedt.Katika wiki za hivi karibuni, wanaharakati wa kundi hilo waliziba barabara kuu, za miji na kuelekea viwanja vya ndege.

Aidha walijifunga kwenye michoro muhimu katika majengo maarufu kama makumbusho kutaka miito yao ya hatua kuchukuliwa dhidi ya athari za mabadiliko ya tabia nchi ishughulikiwe.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents