Burudani
Msanii apoteza fahamu uzushi wa kifo cha Bony Mwaitege (Video)
Katibu Makuu wa Chama cha Waimbaji injili wa Tanzania Madam Stella amekanusha uzushi uliosambaa mitandaoni wa kifo cha muimbaji Bony Mwaitege huku akieleza jinsi rafiki wa muimbaji huyo poteza fahamu baada ya kutumiwa ujumbe na video kwamba rafiki yake huyo amefariki dunia.
Stella amesema msanii huyo wa Injili ni Dastan Mtoi na kwa sasa anaendelea na matibabu Kaloleni Arusha.
Mapema leo asubuhi mitandao ya Kenya ilianza kuripoti tukio hilo na baadae mitandao ya Tanzania kudakia hali ambayo ilisababisha stori hiyo kwenda mbali zaidi na kuzua taharuki kubwa.