BurudaniHabariMuziki

Msanii kutoka Congo ‘Achillian’ aachia album yake ya Conquête 667

Msanii kutoka Uvira, DR Congo, @achillian_ ameachia albamu yake mpya “Conquête 667”, ikiwa na jumla ya nyimbo 13 zenye mchanganyiko wa mitindo ya RnB, Rumba na Afro-pop. Albamu hii ni muendelezo wa safari yake ya kimuziki inayoendelea kuvuka mipaka ya Afrika ya Kati hadi Afrika Mashariki.

Baadhi ya nyimbo zilizopo kwenye albamu hiyo ni ADAM DAKIKA na GOOGLE.

Achillian anaimba kwa Kiswahili, Kifaransa, Kiingereza na Lingala, jambo linalomuwezesha kuwafikia mashabiki wa tamaduni na mataifa tofauti kwa urahisi.

“Conquête 667” ni albamu inayojumuisha ujumbe wa mapenzi, maisha ya kila siku, mafanikio na changamoto, na inathibitisha ukuaji wake kutoka msanii wa Uvira hadi kuwa sauti ya Afrika mpya.

Msanii Achillian

Albamu hii inakuja baada ya mafanikio ya EP ya “Blue Sky” mwaka 2021 na kutwaa tuzo kama Msanii Bora kwenye Lukula Music Awards na Show Ndule Awards.

Sikiliza Conquête 667 sasa kwenye majukwaa yote ya kidigitali.

link hii hapa chini.

https://www.boomplay.com/albums/112195329?from=search&srModel=COPYLINK&srList=WEB

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents