Msanii Rihanna aingia katika orodha ya Mabilionea duniani

Jarida la Forbes limemtaja Rihanna kama mwanamuziki wa kike tajiri zaidi ulimwenguni akiwa na utajiri wenye thamani ya dola bilioni 1.7 sawa na zaidi ya Tsh. Trilioni 3.9 huku kiasi kikubwa cha fedha kikitokana na biashara zake za urembo.

Inaelezwa kuwa zaidi ya dola bilioni 1.4 ambazo ni sawa na Tsh Trilioni 3.2 zinatokana na biashara yake ya urembo (Fenty Beauty) huku Savage X Fenty pekee ina thamani ya dola milioni 270 sawa na Tsh Bilioni 4.8.

Riri amejiunga rasmi na klabu hiyo ya Mabilionea akimfuata Oprah Winfrey kama waburudishaji “entertainer” ¬†wa kike matajiri zaidi duniani.

Bofya hapa kusikiliza.

https://www.instagram.com/tv/CSKIMwlDYo_/

Related Articles

Back to top button