Burudani

Msanii wa muziki Lady Gaga aanguka jukwaani (+video)

Tukio hilo limetoka mara baada ya nyota huyo kumuita jukwaani shabiki wake ambaye anafahamika kwa jina la Jack ili kuungana naye na alipofika ndipo akamrukia mikononi mwake lakini kwa bahati mbaya kijana huyo hakuwa imara na kujikuta wawili hao wakidondoka chini.

Lady Gaga

Kufuatia tukio hilo baadhi ya mashabiki waliyokuwepo kwenye tamasha hilo walifikiri nyota huyo amefariki dunia kutokana na namna alivyolishuhudia. ”Tulifikiri ameaga dunia”.

Alisikika msanii huyo akisema “Kila kitu kipo sawa, kitu pekee ambacho hakipo sawa hapa nikuwa tunahitaji ngazi ya kurudi jukwaani,” Gaga aliyasema maneno hayo huku akisaidiwa kuinuka na walinzi.

Badaye, Gaga alirejea na kutumbuiza kibao chake kiitwacho Million Reasons akiwa sambamba na Jack kisha akishangaa kutokea kwa tukio hilo ”Inashangaza, namna tunavyopendana sana mpaka tunaanguka jukwaani pamoja .” amesema

”Tulivyorukiana mikononi, tulikuwa kama Jack na Rose wa Titanic. Nafikiri tunapaswa kupata kikombe cha chai pamoja.”

https://twitter.com/ThePopHub/status/1185056811126317056?s=20

Pia Nyota huyo alimpa moyo Jack, ambaye alikuwa akilia baada ya tukio hilo.”Usiwe na wasiwasi, kila kitu kiko sawa. si makosa yako,” aliongeza: ”Unaweza kuniahidi kitu? unaweza kuacha kujilaumu kwa kile kilichotokea?”

Mashabiki walikuwa wakifuatilia hali ya Gaga kwa kuwa ana matatizo ya baridi yabisi hali inayomsababishia maumivu makali. Mwaka 2013, aliahirisha onyesho lake la Born This Way baada ya kuteguka nyonga.

https://www.youtube.com/watch?v=dGG8eeiatpg

Baadae kwenye onyesho hilo, Gaga alithibitisha kuwa ajali hiyo haijasababisha madhara yoyote, alipotumbuiza kibao chake, Bad Romance.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents