Msanii wa Nigeria Wadude ameachia ngoma inayoitwa Zanzibar, aeleza sababu ya kuipa jina hilo (+ Video)

Msanii kutoka nchini Nigeria anayejulikana kwa jina la Wadude amewashangaza watu wengi baada ya kuachi ngoma yake inayoitwa Zanzibar.

Mbali ya kuiita ngoma hiyo Zanzibar lakini pia video ya ngoma hiyo ameifanya Zanzibar, akiongea na Bongo5 ameeleza kwa ufupi namna safari na idea ya kuipa ngoma yake jina la Zanzibar.

Wadude amesema kuwa “Safari yangu ya kwanza kusafiri kwenda Zanzibar kama matembezi tu nilikuja na vifaa vyangu vyote vya kurekodi na nikarekodi wimbo wa Zanzibar.”

“Baada ya miezi kadhaa nilipata dm kutoka kwa Sesam kampuni ya usafiri wa majini kutoka Dakar Ghana ambao waliniambia kuwa watathamini wimbo wangu kwa sababu niliimba kuhusu kisiwa kizuri cha Zanzibar. Kisha wakaniuliza ikiwa ningependa kufanya video hiyo. Nikaanza safari yangu kuelekea Tanzania tena, siku tulipoanza kurekodi tuliingia matatizoni na mamlaka kwa sababu hatukulipa ada ya ruhusa na hatukuwa na kibali stahiki”

Wadude ameongeza kuwa “Kamera zetu zilikamatwa na tukawekwa kizuizini, Baada ya maombi mengi tulirejeshewa vitu vyetu lakini ilibidi tupange upya na ilinibidi nirudishe ndege yangu. Tulitumia wiki moja nzima kurekodi video. Sehemu ya video ilirekodiwa katika kisiwa cha nakupenda huko Zanzibar, hivyo ndivyo nilivyofanikisha video yangu na ngoma yangu ya Zanzibar hadi kukamilika.”

 

Related Articles

Back to top button