Msimamo wa Man United kuhusu Jadon Sancho, Cavani

Manchester United bado wanahitaji kumsajili winga wa kulia wa klabu ya Borussia Dortmund, Jadon Sancho wakati wa majira ya joto likiwa kama chaguo lao namba moja. Old Trafford wanaamini pia nyota wao Edinson Cavani ataendelea kusalia kwa msimu mwingine zaidi.

Winga ya kulia ya United imeonekana kuwa katika matatizo msimu na hivyo tumaini lao kubwa limebaki kwa Sancho ambaye wamekuwa wakimtolea macho kwa muda mrefu sasa.

Klabu nyingi barani Ulaya zimeathirika na kuibuka kwa ugonjwa wa virusi vya Corona na kutokuwa na fedha za kutosha katika kufanya sajili zao, lakini Man United imekuwa ikihitaji kujihakikishia usalama wake zaidi katika eneo la ushambuliaji ili kutwaa mataji wamekusudia kumbakiza Cavani.

Sancho is seen as the ideal right wing signing at Old Trafford

Nyota huyo wa Uruguay amekuwa kwenye mafanikio makubwa msimu huu tanngu alipowasili hapo mwezi Oktoba, ameshafunga jumla ya magoli 10 mpaka sasa.

Lakini Cavani amekuwa na mtazamo tofauti kuhusu maisha yake ya baadaye ndani ya Manchester kwakuwa anatamani kumaliza soka lake la kulipwa Amerika ya Kusini licha ya kuwa bado haja fanya maamuzi.

Man Utd are also keen on keeping Edinson Cavani for another year

United inamatumaini makubwa ya kumsajili, Sancho tangu mwaka 2019. Usajili uliyopita Manchester ilishindwa kumsajili nyota huyo ambaye dau lake ni paundi milioni 100.

Klabu hiyo ya Old Trafford haikuwahi kukata tamaa juu ya tumaini lao la kumsajili mchezaji huyo, mazungumzo baini ya timu hizo mbili bado yanaendelea.

Related Articles

Back to top button