Mtoto aliyemeza betri na kukwama kooni afanyiwa upasuaji, madhara gani ymempata ?

Mtoto wa kike wa miezi 11-ambaye alikuwa anakataa kula vyakula vigumu alikuwa kumbe amemeza betri ambayo ilikuwa imekwama kooni kwa kipindi cha miezi minne.

Madaktari walidhani kuwa Sofia-Grace alikuwa na mafindofindo (tonsillitis) au maambukizi ya virusi(viral infection) mpaka alipofanyiwa vipimo vya picha vya X-ray na kubaini kuwa alikuwa na betri ndogo katika koo lake.

Mtoto huyo alifanyia upasuaji wa saa mbili ili kuondoa betri hiyo na sasa anaendelea kula vyakula vya majimaji.

Daktari anasema mtoto huyo amepona kwasababu betri ilikuwa ya zamani na ilikuwa haina nguvu.

Baba yake Calham, kutoka Swindon, aligundua kuwa mtoto wake ana tatizo tangu Januari 2020 na alikuwa anampeleka hospitali kila mara kwa ajili ya matibabu.

Sofia-Grace Hill in hospital

Baba yake alikuwa anahisi kuwa kuna kitu kinamsumbua mwanae zaidi ya ugonjwa alokuwa anaambia hospitali, maana alikuwa anakataa vyakula vizito tu.

Safari nyingine alivyoenda hospitali mwezi Mei, alifanyiwa vipimo vya X-ray ambacho kilionesha kuwa mtoto huyo kuwa amemeza betri ambayo inasababisha madhara makubwa katika afya yake.

Bwana Hill alisema : “Alisikitishwa sana alipoiona na alijikasirikia mwenyewe.

Ninajilaumu mwenyewe lakini nimegundua kuwa hakuna kitu ambacho tungeweza kukifanya kujua kuwa amemeza betri.

Button battery
 

Sofia-Grace alipewa mrija wa kuweza kumsaidia kula chakula na kumfanya aache kukohoa .

Kila ndani ya wiki mbili alikuwa anaenda hospitali kwa ajili ya uchunguzi.

Bwana Hill alisema: “Anaendelea kupata tiba baada ya betri hiyo kuondolewa.

“Lakini najua kuwa atapona baada ya wiki moja na sasa anaendelea kupata nafuu.”

Sofia-Grace Hill and dad Calham
 

Bwana Hill hana uhakika wa jinsi alivyo Sofia-Grace, na sasa ana miaka miwili, kuondolewa kwa betri kooni ni funzo kwa wazazi kuhusu malezi ya watoto na kuweka kwa vitu vya hatari mbali nao.

Alisema yani inabidi kuwafungia, usimpe mtoto wako funguo ya gari lako kucheza nayo.Wazazi ni muhimu kuwa makini zaidi.

Na vyema kushukia kila kitu dhidi ya mtoto wako, mtoto haongei hawezi kujieleza.

“Hospitali na serikali walitoa angalizo la betri kwa muda mrefu.

Lakini si wazazi wote wanafahamu hatari inayoweza kutokea.

Related Articles

Back to top button