HabariSiasa

Mtoto wa mfalme wa Saudi Arabia Mohammed Bin Salman, ateuliwa kuwa Waziri mkuu mpya

Mrithi wa ufalme wa Saudi Arabia, Mohammed bin Salman, ameteluliwa kuwa Waziri mkuu mpya katika mabadiliko ya baraza la mawaziri yaliyotangazwa jana usiku.

Kwa kawaida Mfalme aliyeko madarakani hushikilia wadhifa wa Waziri mkuu. Mohammed bin Salman amekuwa akiangaliwa na wengi kama kiongozi rasmi wa ufalme kwa miaka michache iliyopita.

Awali alishikilia wadhifa wa Naibu Waziri Mkuu zaidi ya cheo chake cha Waziri wa Ulinzi ambacho amekishikilia kwa muda mrefu.

Mwanamfalme huyu mwenye umri mdogo ameleta mabadiliko ya kijamii na na kitamaduni nchini Saudia, lakini anashutumiwa kwa kuanzisha kampeni zinazowalenga watu wanaopinga mawazo yake.

Related Articles

Back to top button