Habari

Mtoto wa miaka minne aendesha gari na kugonga magari kadhaa

Mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka minne huko Uholanzi anaweza kuingia katika mashindano ya magari siku za usoni baada ya kuchukua gari la mama yake kuendesha.

Polisi katika mji wa Utrecht walisema mtoto huyo aligonga magari mawili yaliyokuwa yameegeshwa siku ya Jumamosi, kabla ya kuondoka eneo la tukio akiwa amevalia nguo za kulalia huku akiwa hajavaa viatu.

Watu waliokuwa karibu walipiga simu polisi baada ya kumuona akitembea barabarani peke yake kwenye baridi.

Hakuna aliyejeruhiwa wakati wa kutoroka kwake, huku polisi wakisema kwenye Instagram kuwa wamegundua “Max Verstappen mpya”.

Polisi waliandika kwamba mtoto huyo alifanya tukio hilo siku ya Jumamosi wakati baba yake alipokwenda kazini, na kuchukua funguo za gari la mama yake “ili kwenda kuendesha gari”.

Baada ya maafisa kuitwa kumchukua, taarifa ilikuja ya gari lililotelekezwa karibu na hapo, ambalo lilionekana kugonga magari mawili yaliyokuwa yameegeshwa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents