HabariMichezo

Mtoto wa miaka mitatu aendesha Ferrari SF 90 Stradale (+Video)

Waswahili wana msemo unaosema ‘Mtoto wa Nyoka ni Nyoka’.

Zayn Sofuoğlu mwenye umri wa miaka mitatu (3) ni mtoto wa dereva mashuhuri wa mbio za Magari wa zamani, Kenan Sofuoğlu.

Video bofya HAPA

Mtoto, Zayn amemthibitishia Baba yake kuwa ana uwezo wa kuendesha gari kwa ustadi wa hali ya juu licha ya udogo wa umri wake.

Akiwa kwenye gari la wazazi wake aina ya Ferrari SF 90 Stradale lenye thamani ya dola za Marekani 550,000 mtoto huyo ameonyesha uwezo wa hali ya juu wa kusukuma ndinga.

Kenan Sofuoğlu dereva mstaafu wa mbio za magari ambaye ni baba wa mtoto, Zayn Sofuoğlu kwa sasa ni Mbunge nchini Uturuki.

Imeandikwa na @fumo255

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents