
Russ Cook anapanga kukimbia kilomita 3,000 za urefu wa nchi ya New Zealand.
Mwanamume ambaye alikimbia mbio urefu wote wa Bara la Afrika [kuanzia kaskazini hadi kusini]ameanza hatua yake ya hivi punde ya kukamilisha lengo jipya la kukimbia urefu kamili wa nchi ya New Zealand.
Russ Cook, aliyepewa jina la utani Hardest Geezer, alimaliza shindano lake la awali aliloliita shindano la uvumilivu mnamo Aprili mwaka jana baada ya siku 352.
Mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 27, kutoka Worthing, West Sussex, ana mpango wa kukimbia kilomita 3,000 za Te Araroa Trail, ambapo atakimbia mbio za 60 ultramarathons wakati wa kupanda milima, misitu, ukanda wa pwani na miji.
“Mapokezi ya ajabu na mazuri ambayo nimepata hadi sasa tayari yamenipa taswira ya jinsi ambavyo safari iliyo mbele yangu itakuwa ya kipekee,” alisema.
Ameanza mbio hizo huko Stirling Point, ncha ya kusini ya Kisiwa cha Kusini cha New Zealand – na atakimbia kuelekea kaskazini kwa takriban siku 60 hadi kwenye mstari wa mwisho huko Cape RÄ“inga, Northland.
Bw Cook alisema anatarajia kupanda mara 10 eneo lenye urefu sawa na Mlima Everest katika mwinuko kwa takriban wiki 10 zijazo.
Alisema ana furaha “kurejea barabarani tena” katika msafara wake wa kwanza mkubwa tangu alipokamilisha mbio za urefu wa bara la Afrika.
“Kama kuna jambo lolote, nililojifunza kutokana na uzoefu wangu wa hapo awali barani Afrika, limenifanya nikubali kwamba kuna hatari ninazoziweza na nisizoweza kuchukua ,” alisema.