Habari

Mtunisha misuli kutoka Marekani, Cedric McMillan afariki dunia

Mjenga misuli wa Marekani Cedric McMillan amefariki akiwa na umri wa miaka 44, baada ya miaka kadhaa ya matatizo ya kiafya yaliyosababishwa na Covid-19, na ajali ya barabarani.

McMillan, mkongwe wa muda mrefu wa Jeshi la Marekani na Walinzi wa Kitaifa, alikuwa mjenga misuli mkongwe na mshindi wa 2017 wa taji la kifahari la Arnold Classic.

Kifo chake kilithibitishwa mtandaoni na mfadhili wake, Black Skull USA, ingawa sababu haijawekwa wazi.

Ni kifo cha tatu cha mjenga misuli mashuhuri nchini Marekani katika mwaka uliopita.

“Tunasikitika kuwafahamisha kuwa rafiki na kaka yetu @cedricmcmillan amefariki leo,” Black Skull USA alisema kwenye Instagram. “Cedric atakumbukwa sana kama mwanariadha, mwanachama mwenzetu, rafiki na baba.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents