BurudaniHabari

Muandishi na Mtayarishaji wa muziki Dawda asaini dili Dubai

Muandishi maarufu wa muziki kutoka nchini Gambia Dawda ageukia upande wa uimbaji na kusaini dili nono na kampuni ya usimamizi wa muziki Dubai LPME group.

Dawda katika kazi yake ya uandishi amewahi kuwaandikia wasanii wakubwa kama Sean Kingston,Mohombi,Bayanni,Singah,Iyaz,Charice, Ashley Tisdale n.k

LPME Group ya Dubai kwa sasa inasaini wasanii wanaotokea kwenye tamaduni tofauti tofauti duniani. Katika kuiangazia Afrika, wameanza na Dawda ambae amepata motisha ya kuingia kwenye muziki akisikiliza na kupenda muziki wa Gambia,Senegal,Amapiano ya South Afrika na hata Afro beats ya Nigeria.

Dawda amenukuliwa akisema “Nimekua nikiandika na kutayarisha nyimbo za sehemu nyingi duniani kote, nilipoamua kuanza kuimba mwenyewe nimetaka kuhakikisha naonesha jinsi gani ninajivunia Uafrika wangu,nina furaha kuweza kuwa mbunifu katika kuunganisha kile nilichonacho ndani ya muziki nitakaotoa”.

Dawda ameachia wimbo wake wa kwanza “wine” tarehe 8 mwezi wa 2 ndani ya KIZA,Dubai na anategemewa kuja na EP (Extended playlist) baada ya muda mfupi chini ya uongozi wa LPME Group.

Hatua hii inaashiria mwanga kwa wasanii wa Afrika kuweza kupata nafasi ya kuonekana na makampuni makubwa ya muziki duniani na kufanya kazi nao.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents