Technology

Muda wowote kuanzia sasa Instagram inatangaza mfumo wake mpya wa ‘IGTV’ ni pigo kwa mtandao wa YouTube

Leo Juni 20, 2018 Mtandao wa kijamii maarufu zaidi duniani wa Instagram unatarajiwa kutangaza rasmi mfumo wake mpya wa ‘IGTV’ utakaowaruhusu watumiaji wake kuweka video ndefu hadi dakika 60.

A leaked shot of the video uploading form for Instagram
Muonekano wa video ndefu ikipandishwa Instagram (picha imevujishwa mtandaoni)

Kwa mujibu wa taarifa kutoka mtandao wa Tech Crunch, umeeleza kuwa kwa kuanza Instagram wataanza kuruhusu video za kuanzia sekunde 10 hadi dakika 10, na hii itakuwa ni mahususi kwa Vloggers, waandishi wa habari na wasanii.

Wiki iliyopita mtandao wa Instagram uliripoti kuwa timu nzima ya ubunifu ya mtandao huo imekaa kujadiri namna ya kuongeza urefu wa video zinazopandishwa kwenye mtandao huo.

Mtandao wa habari za teknolojia wa Engadget  umeeleza kuwa video hizo pia zitakuwa na vigezo vya malipo kama ilivyo mitandao mingine kama YouTube n.k .

Kwa sasa mtandao huo unaruhusu video zenye urefu wa sekunde 59 na bado haijawekwa wazi kama huduma hiyo itapatikana duniani kote au laah!!.

Je, ujio wa IGTV huenda likawa tishio kubwa kwa mtandao wa YouTube ambao umejizolea umaarufu duniani kwa kupandishia na kusambaza video?

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents