Muigizaji wa Black Panther Connie Chiume atua Tanzania, atoa mbinu za kutoboa Kimataifa (Video)

Muigizaji nguli wa filamu kutoka nchini Afrika Kusini, Connie Chiume​, ambaye ameshiriki kwenye filamu maarufu Black Panther ametua nchini Tanzania kwaajili ya kutoa mafunzo maalumu ya filamu (Masterclass) jijini Dar es Salaam, Jumamosi ya April 24.

Ijumaa hii baada ya kutua nchini Tanzania alitembelea University of Dar es Salaam (UDSM) katika kitivo cha sanaa na kuzungumza na wanafunzi ambao wapo chuoni hapo.

Muigizaji huyo alitumia fursa hiyo kuwapa picha halisi ya tasnia ya filamu duniani na inataka nini kwa wakati huu na kitu gani sahihi chakufanya ili kuhakikisha Afrika inakwenda mbele zaidi.

Written and edited by @yasiningitu
9

Related Articles

Back to top button