BurudaniUncategorized

Muongozaji wa filamu ya The Karate Kid na Rocky ya ‘Sylvester Stallone’ afariki Dunia

Mtayarishaji na Muongozaji wa filamu za Rocky na The Karate Kid na mshindi wa tuzo za Oscar, John G. AvildsenĀ amefariki dunia.

John G. Avildsen

Mtoto wa John Avildsen aitwaye Avildsen Anthony ameviambia vyombo vya habari leo nchini Marekani kwamba baba yake amefariki kwa ugonjwa wa saratani katika hospitali ya Sinai Medical Senter mjini Los Angeles.

Filamu ya Rocky ilioigizwa na Sylvester Stallone kama bondia aliyejitoa katika ufukara na kuwa tajiri ilikuwa filamu iliouzwa sana mwaka 1976 licha ya kuwa na bajeti dogo kwenye utayarishaji.

Filamu hiyo ilishinda tuzo ya Oscar kwa kuwa filamu bora huku Avildsen akijishindia tuzo ya muongozaji bora.

Rambo kupitia ukurasa wake wa Instagram amethibitisha taarifa hizo kwa kuandika ujumbe uliosomeka ”Muongozaji bora wa Filamu ya Rocky na Mshindi wa tuzo za Oscar John G. Avildsen, RIP nina hakika hivi karibuni utaanza kuelekeza filamu ukiwa peponi’‘.

https://www.instagram.com/p/BVbMGoCDNeU/?taken-by=officialslystallone

Avildsen pia aliongoza filamu ya Karate Kid iliotolewa mwaka 1984 pamoja na Karate Kid awamu ya pili 1986 na Karate Kid awamu ya tatu 1989.

By Godfrey Mgallah

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents