BurudaniHabari

MUSIC VIDEO: MC Joshua – Sitoki bure

Moja kati ya Washereheshaji (MC’s) wanaofanya vizuri hapa Tanzania ni MC Joshua na Good News ni kwamba MC huyo ameamua pia kuingia kwenye muziki wa Injili ambako anaamini kuwa anakipaji pia.

MC Joshua anasema Muziki wa Injili ni huduma kama ilivyo kwa huduma nyingine za kiroho hivyo anaamini muziki wake utaponya wengi.

“Mimi namshukuru Mungu kanibariki kwa vipaji vingi ukitoa kazi yangu ya ushereheshaji (MC’s) pia nina kipaji cha kuimba muziki wa Injili na hii yote ni katika kuburudisha na kutoa huduma za kiroho kwani muziki wa Injili ni tiba pia”, Amesema MC Joshua (@mcjoshuatz).

MC Joshua kwasasa anafanya vizuri na wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la ‘SITOKI BURE’ wenye maudhui ya kuwatia faraja wale wote wanaopitia magumu kwa muda huu, Bofya link hapa chini kutazama video hiyo.

MC Joshua amesema kuwa licha ya kuingia kwenye muziki bado ataendelea pia kufanya shughuli zake za Ushereheshaji (MC).

” Kuingia kwenye Gospel hakunifanyi niache kazi yangu ya awali, Kama kuna mtu ananihitaji kwa shughuli yake nipo sana, Napatikana kwenye mitanfao ya kijamii, Instagram na TikTok natumia @Mcjoshuatz
na kule Facebook na YouTube Chaneli yangu natumia MC Joshua”.

Related Articles

Back to top button