Burudani

Muziki wa Bongo Fleva kuyafikia mataifa 47 Afrika, baada ya Boomplay kuongeza mkataba na Merlin

App inayoongoza kwa huduma ya kusikiliza na kupakua muziki barani Afrika na Merlin ambaye ni mshirika huru wa kutoa leseni ya muziki kidijitali, leo wametangaza upanuzi wa makubaliano ya leseni ambayo yatapanua upatikanaji wa orodha ya muziki kwa wanachama wa Merlin mpaka kufikia nchi zaidi ya 47 barani Afrika.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo Desemba 21,2021 na uongozi wa kampuni hizo kutoka mjini Lagos, Nigeria na London nchini Uingereza.

Mnamo mwaka 2019, Merlin ilitia saini mkataba wa leseni na Boomplay uliojumuisha nchi 11 ambapo kwa sasa Boomplay ina zaidi ya watumiaji hai milioni 60 na jumla ya nyimbo zaidi ya milioni 65.

Programu hiyo tumuishi ndiyo yenye hifadhi kubwa zaidi ya maudhui ya Kiafrika duniani.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kupanuka kwa mkataba wa utoaji leseni wa Boomplay na Merlin kutawapa mamilioni ya wapenzi wa muziki wa Kiafrika katika bara la Afrika upatikanaji wa muziki bora wa ndani na nje ya nchi kutoka katika orodha mbalimbali za wanachama wa Merlin.

Boomplay imekuwa mstari wa mbele kusaidia tasnia ya muziki barani Afrika kuufikia uwezo wake kamili kwa kukamilisha shirikiano zenye mafanikio kupitia lebo na wasambazaji wakubwa duniani sambamba na kusaidia wasanii kikamilifu kupitia promosheni na udhamini mbalimbali, miongoni mwa mambo mengine ni kuwezesha ushirikiano unaolenga kupunguza gharama za data kwa wapenzi au mashabiki wa muziki barani Afrika.

Upanuzi huu pamoja na ushirikiano wa hivi karibuni kati ya Boomplay na Billboard ambao unaorodhesha nyimbo zilizo kwenye App ya Boomplay kama sehemu ya takwimu ya kwenye chati maarufu za Billboard, inathibitisha kujitolea kwao katika kuhakikisha muziki wa Kiafrika unasikika duniani kote.

Muendelezo wa leseni pia unaonesha dhamira ya Merlin ya kuongeza thamani kwa wanachama wake, ikiwa ni pamoja na ufikiaji wa hadhira mpya Afrika yote, huku ikitoa hali bora ya muziki kwa watumiaji wa Boomplay.

Mkurugenzi wa Maudhui na Mikakati wa Boomplay, Phil Choi, amesema “Kadiri idadi ya watumiaji na huduma zetu zinavyokua kwa kasi katika bara zima, ni muhimu kuwa na washirika sahihi ambao mnaweza kuendeleza safari kwa pamoja, na kukuza na kuunga mkono tasnia ya muziki kwa ujumla.

“Kama kiongozi kwenye hakimilizi za muziki ulimwenguni, tunafurahi kwamba Merlin ana maono sawa na sisi na pamoja na faida za Boomplay katika sekta ya muziki wa kidijitali na idadi ya nyimbo zenye ubora wa hali ya juu kutoka Merlin, tunaweza kutarajia ushirikiano wenye hadhi ya kipekee miaka mingi ijayo,”amesema.

Naye Charlie Lexton kutoka Merlin, ameongeza kuwa, “Kupitia ushirikiano huu unaoendelea, watumiaji wa Boomplay katika maeneo mapya yaliyofunguliwa sasa wanaweza kufikia orodha ya nyimbo ya kina ya wanachama wa Merlin kupitia muziki wa ndani na nje ya nchi katika aina zote za muziki paomoja na safu ya lugha. Tunafurahi kuona Boomplay ikikuza ufikiaji wao na kutoa huduma kwa watumiaji wapya kote barani Afrika,”amesema.

Boomplay, ni App inayoongoza kwa huduma ya kusikiliza na kupakua muziki inayomilikiwa na Kampuni ya Transsnet Music Limited. Kampuni ina ofisi Tanzania, Kenya, Ghana, Nigeria, Ivory Coast na Cameroon. App hii inapatikana duniani kote kupitia programu tumishi ya Android na iOS na katika tovuti ya www.boomplay.com

Kwa sasa Boomplay ina zaidi ya watumiaji milioni 60 kwa mwezi (MAU’s) na zaidi ya nyimbo milioni 65.

2021 umekuwa mwaka mgumu. Hiyo ni kweli. Lakini kuna sababu za kuwa wachangamfu tunapoelekea 2022.

-MWISHO-

Kuhusu Boomplay

Merlin ina uwekezaji London, New York, North Carolina, Uholanzi, na Tokyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents