Mvua za Elinino zilivyokwamisha uzalishaji kiwanda cha TPC Kilimanjaro
Mwaka huu kuvuna miwa tani 200,000
MAHITAJI ya sukari hapa anchini yanakadiriwa kuwa ni tani elfu 80,000 hadi 100,000 kwa mwaka jambo lililosababisha baadhi ya wazalishaji kuongeza kasi katika uzalishaji ili kukidhi soko la ndani.
Hapa nchini kumekuwepo na baadhi ya viwanda vyenye kuzalisha bidhaa hii ya matumizi ya kila siku ambapo viwanda hivyo ni pamoja na Mtibwa, Kilombero, Kagera, Bagamoyo na kile cha TPC kilichopo Moshi mkoani Kilimanjaro.
Mfano katika msimu huu wa uzalishaji 2024/2025 katika kuhakikisha kuwa kunakuwepo na uhakika wa sukari kwa kutegemea viwanda vyetu vya ndani kiwanda cha Sukari cha TPC, mkoani Kilimanjaro kimeanza uzalishaji wa sukari ambapo kinatarajia kuzalisha zaidi ya tani 115,000.
Kuongezeka kwa kiwango cha uzalishaji kitaenda kupunguza uhaba wa sukari ambao umekuwa ukijitokeza mara kwa mara na hatimaye kuleta usumbufu kwa watumiaji hao ambapo mara kadhaa wamekuwa wakiuziwa kwa bei ghali hivyo kuchangia ugumu wa maisha.
Mathalani Tanzania ina hekta milioni 44 za ardhi inayofaa kwa kilimo, na asilimia tano tu ndiyo inayolimwa jambo ambalo ni kiwango kidogo sana ikilinganishwa na aina yenyewe ya uhitaji wa mazao ambayo ndio rasilimali kubwa katika viwanda vyetu.
Kwa hapa nchini Tanzania, Sekta ya Kilimo ni muhimili wa maendeleo ya uchumi ambapo kupitia sekta hii inachangia kiasi cha nusu ya pato la taifa, robo tatu ya bidhaa zinazouzwa nje ya nchi na chanzo cha chakula pamoja na utoaji wa fursa za ajira zaidi ya asilimia 75 ya watanzania.
Kilimo kina uhusiano na sekta zisizo kuwa za kilimo kupitia uhusiano wa usafishaji kwenda kwenye usindikaji wa mazao ya kilimo, matumizi na uuzaji nchi za nje, inatoa malighafi kwa viwanda na soko kwa bidhaa zilizotengenezwa.
Tanzania inazalisha takribani asilimia 97 ya mahitaji yake ya chakula. Uzalishaji wa mazao ya chakula unatofautiana mwaka hadi mwaka kutegemea kiasi cha mvua kilichopatikana.
Ni katika kiwanda cha uzalishaji sukari cha TPC kilichopo kaskazini mwa Tanzania kwenye mkoa wa Kilimanjaro umbali wa takribani kilomita 50 kusini mwa Mlima Kilimanjaro hulima hekta 8,000 za mashamba zinazozalisha tani 945,000 za miwa kila mwaka.
Ofisa Utawala Mkuu wa Kiwanda cha Sukari TPC Jafary Ally, amesema kuzalisa sukari kimeanza ramsi uzalishaji baada ya kufungwa kwa muda wa miezi 6 iliyotokona na mvua za elinino na kupelekea mashamba kuujaa maji na kusindwa kuzalisha na hivyo kutofikia malengo.
Anasema tayari miwa imevuna kwa ajili ya uzalishaji na kwamba mwaka jana kiwanda kulizalisha tani 85 kutokana na miezi miwili kuathiriwa na mvua za elinino ambazo zilipelekea mashamba kujaa maji na kushindwa kuvunwa kwa miwa ambayo ilikuwa sahambani., hatua ambayo ilipelekea kiwanda kuzalisha chini ya malengo yaliotarajiwa.
“Miwa ambayo ilikuwa inastahili kuvunwa msimu ule itavumwa msimu huu, hatua ambayo itapelekea kuzalisha sukari nyingi kuliko, kuliko misimu wa nyuma na kuwepo kwa sukari ya kutosha”amesema
Kwa mujibu wa Ally ni kuwa mwaka huu kiwanda cha TPC kinataraijia kuvuna miwa tani 200,000/ ambazo zilishindikana kuvunwa msimu uliyopita ambao ulisababishwa na mvua za elinimo na kuplekea kiwanda kushindwa kufikia malengo.
Amesema msimu huu TPC itakuwa na uzalishaji mkubwa wa sukari kuliko kipindi cha nyuma kutona na kuwepo kwa miwa mingi shambani ambayo haikuvunwa msimu ulipita.
Aidha amesema kwa msimu huu kiwanda kimejiwekea malengo ya kuzalisha tani 115,000 za sukari kuanzia mwezi Juni mwaka huu hadi machi 2025, kutokana na kuwepo kwa miwa mingi shambani na tayari uvunaji umeanza kwa awamu.
“Kama Mungu akipendezwa kiwanda hicho kitakuwa kimezalisha tani 115,000 za sukari ambazo wamejiwekea hadi kufikia mwezi wa machi kufungwa kwa msimu hapo mwakani”alisema
Mkuu huyo wa utawala amesema kuwa kuna changamoto katika soko la sukari kutokana na kuingizwa kwa sukari nyingi hapa nchini kutoka nchi za nje, ambazo hazilipiwi ushuru na kwamba itakuwa na utofauti wa bei ya sukari inayozalishwa hapa nchini na ile ya nje ya nchi.
Kwa kile kilichoelezwa ni kutafuta uhai kwa viwanda vya ndani ni kuwa kiwanda kiko katika maongezi na serikali kuhakikisha sukari inayozalishwa ndani inapata soko sambamba na ile iliyotoka nje ya nchi.
Hata hivyo kunaweza kuwepo kwa sukari ya kutosha kuliko miaka ya nyuma kutokana na viwanda vya sukari nchini vyote kuanza uzalishaji pia kuwepo kwa kiwanda kingine kipya cha sukari ambacho kimeanza uazalishaji.
Kwa mantiki hiyo viwanda vyote vikizalisha sukari nchi itakuwa na sukari ya kutosha na kuokoa fedha za kigeni ambazo zimekuwa zikitumia kuagiza sukari nche ya nchi.
Godson Mmasy mkazi wa Moshi na mfanyabiashara wa vyakula alisema ipo haja kuangaliwa upya hali ya uingizwaji sukari kwani tayari kumeshaanza kuwa tishio kwa wazalishaji wa ndani.
“Unajua sukari inayotoka nje mbali na kuwa haitozwi ushuru lakini pia bado wanaiuza kwa bei rahisi ukilinganisha na hii ambayo inazalishwa hapa nchini,” amesema
Amesema kutokana na hali ilivyo wafanyabiashara wasio waaminifu hufunga sukari kutoka nje ya nchi katika vifungashio vya kiwanda cha TPC jambo linaloleta udanganyifu lakini wananchi wakinunua kwa kulaghaiwa huku TPC wakibaki na mlundikano wa sukari ambayo imekosa wateja
Written by Janeth Jovin