Habari

Mvuvi asimulia alivyomezwa na Nyangumi

Kumezwa, kutapikwa na kurejeshwa nchi kavu: Hadithi ya ajabu ya mwanaume aliyekwama mdomoni mwa nyangumi na kunusurika.

Michael Packard en el hospital, el 11 de junio de 2021

Mvuvi nchini Marekani alimezwa na nyangumi na kutapikwa ndani ya maji dakika chache baadaye wakati alipokuwa akipiga mbizi baharini.

Michael Packard anasema kuwa alikua akipiga mbizi wakati alipojipata ghafla ndani ya mnyama huyo mkubwa wa baharini kwa sekunde 30 hadi 40 kwenye eneo lililopo ufukweni mwa mji wa Provincetown, Massachusetts.

Mnyama huyo alimtema Packard, mbaye magoti yake yalikuwa tayari yameteguka.

Licha ya mke wake kumuomba abadililishe kazi, Packard anasema hana nia ya kuiacha kazi yake ya miaka 40 kama mpiga mbizi kwenye eneo la Cape Cod, mlango bahari uliopo eneo mashariki mwa jimbo la Massachusetts.

Jamii ya nyangumi aina ya Humpback ambao huwa na urefu wa hadi mita 15 pia wanaweza kuwa na uzito wa karibu tani 36.

Ballena jorobada

Kulingana na Shirika la World Wide Fund for Nature, idadi ya nyangumi hao inakadiriwa kuwa 60,000.

Packard, mwenye umri wa miaka 56, aliliambia gazeti la Cape Cod Times la Massachusetts kwamba yeye na wenzake walikuwa wamekwenda na boti lao katika ufukwe wa Herring Cove beach Ijumaa asubuhi, ambako hali ilikuwa shwari kabisa ambako maji yalikuwa na urefu wa takriban kina cha mita 6 kwenda chini.

Baada ya kuruka ndani ya maji alihisi ”amepigwa na kitu kikubwa na mara kila kitu kikawa cheusi”, Packard aliiambia WBZ-TV News.

“Anajaribu kunimeza “

Mvuvi huyo alihisi kuwa alikuwa ameshambuliwa na mmoja wa papa wakubwa weupe ambaye huogelea katika eneo hilo. “Halafu nikahisi kana kwamba sina meno pande zote,”alisema.

“Halafu nikagundua , ‘Oh Mungu wangu , Niko ndani ya domo wa nyangumi na anajaribu kunimeza. Kweli, nitakufa.’

Bw Packard anasema alipokuwa ndani ya mdomo wa nyangumi aliwafikiria mke wake na watoto wake wawili wa miaka 12, na 15.

Ballena jorobada

“Halafu ghafla alinitapika nje … na kuanza kutikisa kichwa .”

“Alinitupa hewani na nikaanguka ndani ya maji. Nilikuwa huru basi nikaelea pale. Sikuamini yaliyonisibu… Niko hapa kusimulia.”

Wapiga mbizi wenzake aliokuwa nao kwenye boti, ambao walikuwa wakihangaika walau kuona mapovu ya pumzi ya oksijeni kutoka kwenye kifaa cha kupumulia cha Bw Packard, walimvuta na kumuingiza ndani ya boti.

Idara ya zima moto ya Provincetown imekithibitia chombo cha habari cha CBS New kwamba walipokea simu iliyowaita majira ya saa sita na robo ikiwaomba waje kumsaidia mvuvi na mpigambizi kwenye ufukwe Provincetown.

Ilikuwa ni kwa bahati mbaya

Ni nadra sana kwa nyangumi kummeza binadamu,wanasema wanasayansi.

Nyangumi wenye maumbile makubwa kwa kawaida kupanua midomo yao sana wanapotaka kupata mlo ili kuwameza samaki wengi iwezekanavyo.

Matokeo yake, wanasayansi wa majini wanaamini kuwa kilichotokea kwa Bw Packard kwa vyovyote ni ajali.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents