Mwabukusi: TLS haijalamba asali, inafanyakazi ya kuisaidia jamii

RAIS wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Wakili Boniface Mwabukusi amesema kuwa chama hicho kipo kwa ajili ya kusaidia wananchi na wanapofanya kazi kwa kushirikiana na Serikali siyo wanakuwa wamelamba asali kama watu wengine wanavyosema.
Mwabukusi ametoa kauli hiyo jijini hapa leo Februari 3,2025 katika viwanja vya Chinangali alipokuwa akitoa taarifa yake mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hasani wakati wa maadhimisho ya kilele cha wiki ya Sheria yenye kauli mbiu isemayo “Tanzania ya 2050 Nasafi ya taasisi zinazosimamia haki madai katika kufikia malengo makuu ya dira ya Taifa ya Maendeleo”.
Amesema kuwa chama hicho kipo kwaajili ya kusaidia jamii kupata haki bila upendeleo wa aina yeyote na kwamba wataonya, kukemea, kushauri na kupongeza kama itabidi kwa ajili ya manufaa makubwa ya nchi na siyo chama cha siasa.
Aidha Mwabukusi ameishukuru Wizara ya Katiba na Sheria kuwatupatia gari na kueleza kuwa gari hiyo litatumika kwa ajili ya kufanya kazi ya kutafuta haki kwa watu ambao wanahitaji msaada wa kitaifa.
“Unakuta mtu analalamika TLS kupewa gari,TLS haipokei rushwa ni chama ambacho kinasimamia sheria na hakipo kwa ajili ya kufanya utabiri wala kufurahisha watu wa upande mmoja na kukandamiza upande mwingine bali sheria inasimawa kwa watu wote,”amesema Mwabukusi
Written by Janeth Jovin