Habari

Mwaka mmoja jela ukitembea nje ya ndoa – Indonesia

Bunge la Indonesia limepitisha sheria iliyofanyiwa mageuzi ililiyokuwa ikisubiriwa muda mrefu ambayo inavitazama vitendo vya zinaa kwa raia na wageni wanaoitembelea Indonesia kuwa kosa la uhalifu.

Sheria hiyo mpya yenye utata ambayo imeidhinishwa na bunge inapaswa kusainiwa na rais kwa mujibu wa naibu waziri wa sheria na haki za binadamu nchini humo Edward Hiariej.

Naibu waziri huyo amesema sheria hiyo haitotekelezwa mara moja na inaweza kuchukua mpaka miaka mitatu kuondokana na sheria ya zamani na kutekeleza mpya.

Kwa mujibu wa marekebisho yaliyofanywa, mtu anaweza kukabiliwa na kifungo cha mwaka mmoja jela kwa kushiriki ngono nje ya ndoa. Ingawa mashitaka yanayohusu zinaa yanapaswa kuzingatia ripoti za polisi zilizowasilishwa na wanandowa, mzazi au mtoto.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents