HabariMichezo

Mwamba gani wa Kariakoo ametisha kwenye usajili..?

YANGA SC kwenye dirisha hili la usajili limefanya maboresho safu yake ya ushambuliaji kwa kumuongeza Kennedy Musonda jezi namba 25, historia ikionekana kumbeba huko atokako Zambia akiwa na mechi 17 amefunga magoli 11.

Sehemu ya kiungo ya Wananchi nayo haikusahaulika, wakamuongeza Kiungo ‘Chuma’, Mudathir Yahya ambaye uwezo wake wa kutukuka awapo uwanjani wadau na mashabiki wa soka wanaufahamu.

Ulinzi ni moja kati ya kitu muhimu ndipo wakamsajili Mamadou Doumbia huku waliowengi wakihusisha usajili huu na kipa wao Djigui Diarra kama mchora ramani mpaka kufikiwa kwa mchezaji huyo.

Inadaiwa taarifa za kuumia kwa kipa namba mbili wa kikosi hicho, Aboutwalib Mshery mbele ya benchi la ufundi ndiyo ikafungua milango kwa Metacha Mnata kuja kuimarisha lango.

SIMBA SC akashusha Mbabe wa Mayele, huyu ni Jean Toria Baleke msimu wa 2020/21 Ligi Kuu ya pale Congo huyu BALEKE alifunga Magoli 14 na kumzidi Fiston Mayele ambaye kwa sasa yupo Yanga, hawa ni wachezaji wanaojuana vizuri tu.

Baleke kabla ya kutua TP Mazembe alikuwa anaongoza kwa Ufungaji ligi kuu akiwa na magoli tisa (9) mechi 14 akiwa na Sports Youth of Kishansa(JSK) hii ni ‘Mashine’ kweli.

Mshambuliaji Mohammed Mussa huyu ukiachia mbali nyota yake kung’aa Mapinduzi Cup akiwa na Mlandege FC lakini pia ni kati ya wafungaji wanaoongoza kwa Magoli saba (7) Ligi Kuu Zanzibar (ZPL).

Ismael Sawadogo kiungo mkabaji mwenye kutumia mguu wa kushoto zaidi, kiungo mkabaji sio minguvu pekee sasa hivi anatakiwa pia kusaidia timu kushambulia, kufunga ikiwezekana na kuasist huyu ni Gifted player.

Saido Ntibazonkiza na matunda yake Simba SC yameshaanza kuonekana na profile yake ni kubwa mno hatuta maliza.

Timu gani ya Kariakoo imefanya usajili wa kutisha dirisha hili …?

Imeandikwa na @fumo255

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents