Michezo

Mwamuzi wa kati Yanga vs Simba Jumamosi ya Aprili 30, atangazwa

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limewatangaza Maafisa watakaosimamia mchezo namba 160 wa Ligi Kuu ya NBC baina ya Yanga SC dhidi ya Simba SC siku ya Jumamosi ya Aprili 30, 2022.

TFF imemtangaza Ramadhan Kayoko kuwa ndiye mwamuzi wa kati kwenye mchezo huo wa Derby ya Kariakoo siku ya Jumamosi ya Aprili 30.

Kayoko ndiye aliyechezesha mchezo wa Ngao ya Jamii baina ya Simba na Yanga ambapo Wananchi walishinda 1 – 0 dhidi ya Mnyama.

Refa huyo ndiye aliyechezesha mchezo wa kimataifa wa kirafiki wa kuadhimisha tukio la Wiki ya Mwananchi uliofanyika Agosti 29 ambao Yanga ilipoteza kwa mabao 2-1 dhidi ya Zanaco ya Zambia.

Lakini pia Kayoko ndiye aliyechezesha mechi ya kuadhimisha kilele cha Tamasha la Simba Day, Septemba 19 ambao Simba ilichapwa bao 1-0 na TP Mazembe ya DR Congo.

Related Articles

Back to top button