Burudani

Mwana FA aanza kuwakimbiza mchakamchaka, atoa maagizo

Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma @mwanafa ameagiza makampuni na maeneo yanayotumia kazi za Sanaa na ubunifu kujinufaisha kibiashara kuhakikisha kuwa yanalipa mirabaha na madeni ya nyuma yanayodaiwa huku akiiagiza Ofisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA)
iwachukulie hatua za kisheria ikiwemo kuwafikisha Mahakamani wote waliokaidi kulipa.

Me. Hamis Mwinjuma ametoa maagizo hayo leo Machi 16, 2023 alipofanya ziara ya kikazi katika ofisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA) kwa ajili ya kujionea shughuli zinazofanywa na ofisi hiyo.

Hatua hiyo inakuja baada ya COSOTA kuwasilisha taarifa inayoonesha kuwa baadhi ya makampuni nchini yamekuwa yakikaidi kwa makusudi kulipia mirabaha huku yakiendelea kutumia kazi za Sanaa katika biashara zao.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents