Burudani

Mwana FA afungua mwaka kikazi na Wakuu wa Idara Muheza

Mbunge wa Muheza, Hamis Mwinjuma ( @MwanaFA ) amekutana na Wakuu wote wa Idara na vitengo ndani ya Halmashauri ya wilaya ya Muheza katika kikao alichokiitisha kwa wilayani humo.

 

Lengo kuu la kikao ilikua ni pamoja na kuweka mikakati ya pamoja na kujadili changamoto zinazojitokeza kwenye Majukumu ya kila siku ya kuwatumikia wananchi wa Jimbo la Muheza.

 

Katikati ya Kikao hicho cha Mwana FA na watendaji wenzake walipata ugeni wa ghafla wa Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tanga Bw Rajab Abdulrahman ambapo aliwasalimia na kuacha nasaha zake ikiwa ni katika kuhakikisha ilani ya Chama cha Mapinduzi, Chama chenye dhamana ya kuwatumikia wananchi kwa sasa, inatekelezwa kwa ufanisi.

 

Wengine ni waliohudhuria Kikao hiki ni pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri na Sektetarieti ya CCM ya Wilaya ikiongozwa na Katibu wa CCM wilaya Ndugu Simon Leng’ese.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents