Habari

Mwanafunzi Chuo Kikuu KCMC ashinda Nissan Dualis ya Benki ni Simbanking

Benki ya CRDB leo imemtangaza Hussein Hamisi Hamadi (23) ambaye ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha KCMC kuwa mshindi wa pili wa gari aina ya Nissan Dualis katika kampeni yake ya Benki ni Simbanking.

Hussein anayesomea shahada ya Fiziolojia chuoni hapo ameibuka mshindi katika droo iliyochezeshwa leo, tarehe 10 Julai 2024 makao makuu ya Benki ya CRDB. Ameibuka mshindi wa gari hilo kutokana na miamala mingi aliyoifanya kwa kutumia simu yake ya mkononi ndani ya miezi mitatu iliyopita mpaka Juni 30.

Droo hiyo iliyoongozwa na Meneja Mwandamizi wa Huduma za Benki za Kidijitali wa Benki ya CRDB, Mangire Kibanda ni ya pili ya kutoa gari ambayo hufanyika kila baada ya miezi mitatu huku washindi wa bajaji na bodaboda wakipatikana kila mwezi sambamba na wanafunzi wa vyuo vikuu wanaojinyakulia kompyuta mpakato.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents