Habari
Mwanamke Initiatives Foundation kudhamini mashindano ya Ndoyamle Cup
Katika kudumisha Muungano wa Taifa kupitia michezo Taasisi ya Mwanamke Initiatives Foundation imetangaza kudhamini mashindano ya Ndoyamle Cup yanayohusisha mabingwa wa michuano ya Ndondo Cup ya Tanzania bara na Yamle Yamle Cup ya Visiwani Zanzibar
Sadie Ally Flash ni Mwenyekiti wa YamleYamle Cup,Edgar Kibwana ni Mwakilishi wa upande wa Ndondo Cup na Fransic Forodha ambaye ni mwakilishi wa Mwanamke Initiatives Foundations wanazungumzia juu ya shindano hilo.