FahamuHabari

Mwanamke miaka 29 akamatwa kwa kujifanya mwanafunzi wa Sekondari

Mwanamke mwenye umri wa miaka 29 amekamatwa huko New Jersey kwa madai ya kujifanya mwanafunzi wa shule ya sekondari.

Mwanamke huyo aliyetambuliwa na polisi kwa jina la Hyejeong Shin ameshtakiwa kwa kutumia kitambulisho feki kujiandikisha katika Shule ya sekondari ya New Brunswick.

Bi Shin alihudhuria shule hiyo kwa siku nne kabla ya wafanyakazi wa shule hiyo kugundua umri wake.

Maafisa wa shule walisema polisi wanachunguza suala hilo, na jinsi mchakato wa uandikishaji wa shule za wilaya unavyofanyika.

Suala hilo lilibainishwa katika mkutano wa bodi ya elimu wa eneo hilo mnamo Jumanne, ambapo Msimamizi wa Wilaya wa shule ya umma New Brunswick, Johnson aliwaambia waliohudhuria kuwa Bi Shin alikamatwa akiwa shuleni.

“Wiki iliyopita, aliwasilisha hati za uongo, mwanamke huyo aliyejifanya mwanafunzi aliweza kusajiliwa katika shule yetu ya sekondari,” Bw Johnson alisema.

Aliongeza kuwa amekuwa katika madarasa kadhaa na alitumia muda na wataalamu wa ushauri ambao walijaribu kupata taarifa zaidi kumhusu.

Umri wa uongo wa Bi Shin ulifichuliwa, Bw Johnson alisema, na shule iliarifu polisi mara moja.

Tangu alipokamatwa kwa kukabidhi cheti cha uongo cha kuzaliwa “kwa nia ya kujiandikisha kama mwanafunzi wa shule ya sekondari”, Idara ya Polisi ya New Brunswick imesema.

Wanafunzi walisema kuwa mwanamke huyo alikuwa amewatumia ujumbe baadhi yao, akiwataka washiriki.

Sheria ya jimbo la New Jersey inaruhusu wanafunzi kuandikishwa shuleni hata bila mlezi au bila karatasi zote zinazohitajika, polisi walisema.

Hii si mara ya kwanza kwa mtu mwenye umri wa makamu kukamatwa kwa kujifanya mwanafunzi wa shule ya sekondari.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents