FahamuHabari

Mwanamke wa Nigeria Hilda Baci, aweka rekodi duniani

Mpishi wa Nigeria, Hilda Effiong Bassey, almaarufu Hilda Baci, ameweka rekodi na kumpita anayeshikilia rekodi hiyo ya dunia ya Guinness kwa sasa ya kupika muda mrefu zaidi.

Kwa ustadi wake, Hild amevunja Rekodi ya Dunia ya Guinness kwa kutumia muda  mdefu zaidi wa kupikia  baada ya kufikia saa 87 dakika 50.

Ndani ya Mgahawa huo alianza shindano hilo siku ya Alhamisi baada ya kuwasha jiko lake saa kumi jioni na kumpita anayeshikilia rekodi ya dunia kwa sasa Jumatatu ya leo asubuhi.

Iwapo atathibitishwa na Rekodi ya Dunia ya Guinness, atampita anayeshikilia rekodi ya dunia kwa sasa, Lata Tondon, mpishi wa Kihindi aliyefanikisha kazi hiyo mwaka wa 2019 kwa kutumia saa 87 dakika 45 akirekodi kupika bila kukatizwa.

Mbio za kupikia za Baci kwa sasa zinaendelea katika Amore Gardens huko Lekki, Jimbo la Lagos.

Katika jaribio lake linaloendelea la kuvunja rekodi, Wanigeria, wakiwemo watu mashuhuri kadhaa walivumilia mvua ili kumshangilia mpishi huyo aliyeonekana kuchoka.

Baadhi ya masharti ya kuvunja rekodi hiyo ni kama yafuatayo:

# Sharti la kwanza ni kwamba, Simama ukiwa unapika, Hutakiwi Kukaa, #- sharti la pili, Hautakiwi Kutumia Kahawa Au Kinywaji Chochote Cha Kuongezea Nguvu #- Ruksa Kunywa, Kula Na Kutumia Glucose, #- Siku 4 Bila Kulala ukiwa unapika, #- Dakika 5 Tu Za Kupumzika Kila baada ya saa moja, #- Kila utakachopika unapaswa ugawe Bure Chakula Kwa Wateja Na Sio Kuwauzia, #- Kupika Chakula Cha Aina Yoyote Ile unachopenda Wala Hakuna Sheria Ya Kumpangia Chakula Cha Kupika, #- Kila Chakula utakachopika Na Kila Sahani utakayo toa Kwa Mteja Inawekwa Kwenye Rekodi Kama (Kumbukumbu)

Wewe ungweza masaa mngapi??

Mastaa kama Wizkid, Burna Boy, Tiwasave na wengine wamempongeza na Tiwa ameenda kumtembelea kwenye mgahawa wake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents