Mwanasiasa wa upinzani Rwanda amekamatwa kwa madai ya ubakaji

Mwanasiasa wa upinzani nchini Rwanda ambaye ni mwalimu wa chuo kikuu Christopher Kayumba ameshikiliwa kwa madai ya ubakaji.

Bwana Kayumba aliheshimu wito kutoka kitengo cha uchunguzi siku ya Alhamisi.

Ofisi hiyo ya uchunguzi ilisema imefunga imemaliza kufanya uchunguzi na inamkabidhi kusikilizwa mashtaka yake.

Kiongozi wa chama cha jukwaa la demokrasia yaani Rwandan Platform for Democracy (RPD) alishutumiwa madai ya ubakaji siku chache baada ya kuzindua chama chake.

Amekanusha madai hayo dhidi yake na kusema wana nia ya kumuharibia taswira yake kwa umma pamoja na ya chama chake. Miongoni mwa watu wanaomshutumu ni mwanafunzi wake wa zamani

Related Articles

Back to top button