Habari

Mwandishi wa Millard Ayo Eugen Peter apatikana Muhimbili

Mwandishi wa Habari Eugen Peter ambaye leo asubuhi kupitia kurasa za @millardayo alitangazwa kutokujulikana aliko, amepatikana mchana huu akiwa amelazwa katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI), Dar es salaam.

Kwa mujibu wa MOI, Eugen alifikishwa Hospitali hapo December 31,2024 akitokea Hospitali ya Mwananyamala akiwa amepoteza fahamu na akiwa na majeraha mikononi na kichwani yanayotajwa kuwa yamesababishwa na ajali ya pikipiki ambapo alilazwa kama Mgonjwa asiyejulikana utambulisho wake ( unknown ).

Eugen ambaye wakati wa kutoweka kwake alikuwa amechukua likizo ya kazi mwishoni mwa mwezi December, hakwenda nyumbani kwao Arusha kama ilivyotarajiwa wala hakuonekana nyumbani kwake Ubungo na simu zake hazikuwa zikipatikana ndipo Ndugu, Jamaa na Marafiki wakishirikiana na Ofisi yake (AyoTV) walipoanza kumtafuta katika maeneo mbalimbali.

AyoTV inawashukuru wote walioshiriki katika jitihada za kumtafuta na wale wote waliofanikisha kupatikana kwake ikiwemo Taasisi ya MOI.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents