Habari

Viongozi wamiminika kuuaga mwili wa Lowassa Karimjee

Viongozi wamiminika kuuaga mwili wa Lowassa Karimjee

Mamia ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam na viongozi mbalimbali wamemiminika katika viwanja vya Karimjee kwa ajili ya kuuaga mwili wa aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa.

Lowassa alifariki dunia Februari 10, 2024 katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu baada ya kuugua ugonjwa wa shindikizo la damu, utumbo kujikunja na mapafu kujaa maji.

Miongoni mwa viongozi waliojitokeza leo kuuaga mwili wa kiongoni huyo, Makamu wa Rais wa Tanzania Dk. Philip Mpango, Rais wa Zanzibar Dk.Hussein Mwinyi, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ni Rais Mstaafu wa awamu ya Nne, Jakaya Kikwete, Rais Mstaafu wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein, MaWaziri wakuu wastaafu Jaji Joseph Warioba na Fredrick Sumaye.

Wengine ni Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Francis Mutungi, Mkuu wa Polisi Mstaafu Omary, Mahita, waliowahi kuwa mawaziri William Ngereja, Andrew Chenge pamoja na wake wa marais wastaafu Mama Salma Kikwete pamoja na Mariam Mwinyi.

Viongozi wengine ni Waziri wa Maji Jumaa Aweso, Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa, Waziri wa Afya Ummy Mwalimu, Katibu Mkuu wa UWT Jokate Mwegelo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila pamoja na Mkuu wa Wilaa ya Kigamboni Halima Bulembo.

Tizama video nzima katika akaunti ya youtube ya Bongo 5 inayoonyesha Mwili wa aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa ulivyoingia kwenye Viwanja vya Karimjee kwa ajili ya kuagwa.

Endelea kuwa karibu nasi kwa mutukio yote yanaondelea juu ya msiba huu mzito

Written by Janeth Jovin

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents