Habari

Mwili wa Mtanzania aliyefia vitani Ukraine umewasili Tanzania alifajiri ya leo

Ndugu na jamaa wa Mtanzania Nemes Tarimo wamepokea mwili wa kijana huyo leo alfajiri katika uwanja wa ndege wa Jijini Dar es salaam.

Kwa mujibu wa familia, kijana huyo ataagwa kisha kusafirishwa kwa ajili ya maziko Nyanda za juu kusini mwa Tanzania.

Mapema wiki hii serikali ya Tanzania ilithibisha kijana huyo kuuawa vitani Ukraine mara baada ya kufungwa kwa uhalifu nchini Urusi na baadae kujiunga na kundi la mamluki wa Urusi , Wagner.

Nemes Tarimo alienda nchini Urusi kwa ajili ya masomo ya juu kabla ya kupatwa na umauti wake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents