Michezo

Nabi alia Kumkosa Mzize: Afrika kuna Washambuliaji 6 tu.

Kocha Mkuu wa Kaizer Chief, Nasreddine Nabi amesema kuwa Bara la Afrika lina uhaba wa washambuliaji jambo linalofanya Vilabu vingi kugoma kuwauza washambuliaji wao kwa timu nyingine.

Nabi ambaye amewahi kuifundisha Yanga SC kwa mafanikio makubwa amesema hayo baada ya Ofa yake ya kumtaka mshambuliaji kinda wa Yanga, Clement Mzize kukataliwa na uongozi wa klabu hiyo.

“Kusema kweli Soko la washambuliaji ndani ya Afrika kwasasa ni gumu, tujaribu kufatilia kama tungempata Mzize lakini klabu yake ilitia ugumu kwa sababu inamuhitaji.

“Kwa sasa ndani ya Afrika kuna Washambuliaji 6 tu ambao ni hatari na hakuna klabu hata moja kati ya zinazowamiliki ambazo zipo tayari kuwauza.

“Nahitaji angalau Miezi Miwili ya kufanya Scouting ya washambuliaji ili kumleta ndani Kaizer Chiefs na akafunga Magoli mengi” amesema Nabi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents