Naibu Waziri atamani uchaguzi ili kuheshimiana mbele ya Rais Samia

Naibu Waziri wa Afya, Dk. Godwin Mollel, amesema akimtazama Rais Samia Suluhu Hassan anatamani uchaguzi uwe kesho ili watu waheshimiane mjini.

Mbunge Godwin Mollel

Akizungumza leo mbele ya Rais amia, Mh. Mollel ambaye ni Mbunge wa Siha amesema kutokana na uongozi wa Rais huyo wanatembea kwa kuringa.

Akizungumzia namna serikali ya Rais Samia inavyopeleka maendeleo kwenye mkoa wa Kilimanjaro, Mh. Mollel amesema kwamba haijawai kutokea kwa Mkoa wa Kilimanjaro kwa hospitali mbili (Mawenzi na KCMC) kupatiwa Bilion 11.3.

Mh. Mollel ameongeza kwamba kwa kipindi kifupi cha uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan kwenye Wizara ya Afya, ametoa fedha za kwa ajili ya CT Scan 29 nchi nzima ambapo kabla ya uongozi wake zilikuwepo mbili tu, huku akisisitiza viwanda vya kuzalisha hewa tiba vilikuwa vinne 4 lakini “yeye katika kipindi chake tunaenda kuwa na viwanda 51 vya kuzalisha hewa tiba nchini”.

Nikimuangalia Mama yetu napata hamu uchaguzi uwe kesho ili tuoneshane hapa mjini, tunyooshane tuheshimiane hapa mjini au nyie mnasemaje? Tunaringa tupo na wewe mama yetu” Godwin Mollel.

BY: Fatuma Muna

 

Related Articles

Back to top button