Habari

NALA yaiunganisha Afrika na Ulaya (Video)

Kampuni ya kimataifa iliyozaliwa Tanzania (NALA), inayoshughulika na mfumo wa malipo, duniani na kampuni ya Teknolojia na Mawasiliano ya Vodacom Tanzania PLC kupitia M-Pesa leo wametangaza usihirkiano mpya utakaoiwezesha huduma ya kutuma na kupokea pesa kimataifa (IMT), kusogeza huduma zake kwa wateja walioko nchi za Umoja wa Ulaya (EU) kutuma na kupokea pesa kirahisi, haraka na kwa gharama nafuu.

Kampuni ya NALA, ambayo ni taasisi ya huduma za kifedha kidijitali (Fintech company), imetanua huduma zake katika bara la Ulaya kwa kuongeza nchi 19 zilizoko barani humo baada ya kuanza kutoa huduma katika nchi za Marekani ikitokea Uingereza. NALA ina nia ya kuiunganisha Dunia kwa kuwawezesha Waafrica wanaoishi nchi za Ulaya kutuma pesa Tanzania nan chi nyingine za Africa. Kwa kushirikiana na Vodacom M-Pesa, upanuzi huu unaongeza umuhimu wa kutuma na kupokea pesa kwa haraka na gharama rahisi kupitia huduma hii.

Vodacom M-Pesa  ni mtandao mkubwa wa huduma za kifedha nchini Tanzania, hapo hapo NALA anakuja kama mshirika wa muhimu sana katika wakati huu ambapo huduma za kifedha ziko kiganjani. Kampuni hizi mbili zina lengo moja la kuhakikisha utumaji pesa unakuwa wa haraka, salama, wenye kuaminika na wenye gharama nafuu hapa nchini. Ushirikiano huu wa kihistoria unaongeza matokeo chanya kwa kampuni za Kiafrica na kuzirahisishia mifumo yake ya malipo.

Pamoja na kuwa na mifumo mingi ya utumaji pesa kuja Africa kutoka mabara mengine, Bara la Africa limebaki kuwa ni sehemu yenye gharama Zaidi kutuma pesa. Benki ya Dunia inaeleza kwamba gharama ya kutuma pesa ni wastani wa asilimia 9 ya kile unachotuma, zaidi mifumo mingi iliyopo imekuwa na ada/gharama zilizojificha na hivyo kukosekana kwa gharama halisi ya utumaji pesa. NALA imekuwa ikifanyia kazi juhudi za kubadilisha namna utuma ji wa pesa unavyofanyika kwa kuleta huduma za wazi za kifedha.

 Afisa Mtendaji Mkuu na Mwanzilishi mwenza wa NALA Benjamin Fernandes alisema, “nikiwa ni Mtanzania, inanipa Furaha kuwafikia robo ya Waafrica wenzangu wanaoishi Ulaya kwa kuwapa huduma rahisi na ya kuaminika ya kutuma pesa nyumbani. Kupitia Vodacom M-Pesa tunaiunganisha miundombinu na hivyo kuleta daraja la malipo kati ya nchi za Uingereza, Marekani na jumuiya ya Ulaya na Tanzania. NALA imekuwa kwa haraka Zaidi na kuongeza wigo wake kijiografia, kupitia bidhaa na pia kwa kuboresha miundombinu yetu. Ushirikiano tuliozindua leo na M-Pesa ya Vodacom utatuwezesha kuongeza wigo wa kutuma na kupokea pesa kutoka nchi nyingi Zaidi duniani, kwa pamoja tunaendeleza nia yetu ya kuleta fursa za kiuchumi kwa waafrika pote duniani.”

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa M-Commerece, Epimack Mbeteni, aliupongeza ushirikiano huo huku akiongeza kwamba unaendana na mipango ya kampuni katika kukuza huduma ya utumaji pesa kimataifa (IMT). Wateja wa Vodacom M-Pesa sasa wanaweza kutuma na kupokea pesa kutoka nchi zaidi ya 200 moja kwa moja kwenda kwenye akaunti zao za M-Pesa.

“Tumetumia ubunifu na ushirikiano wetu ili kuhakikisha tunawezesha utumaji na upokeaji pesa kimataifa katika bara la Afrika na dunia kwa ujumla na hivyo kuiwezesha dunia kutuma pesa kirahisi zaidi na hivyo kuwezesha biashara kati ya mipaka ya nchi. Tunaendelea kuongeza faili letu kwa kupitia ushirikiano na makampuni mbalimbali, tunafuraha kushirikiana na NALA kampuni ambayo inatokea hapa hapa nchinilakini inabadilisha namna na jinsi ya kutuma pesa duniani.”

Ushirikiano huu utaambatana na kampeni itakayowazawadia wateja wa NALA na M-Pesa pindi watakapotumia huduma hii. NALA iatwazawadia wateja wapya kiasi cha $10 pindi watakapotuma kwa mara ya kwanza, lakini pia kutakuwa na nafasi ya kujishindia tiketi mbili za ndege (kwenda na kurudi) kwa wateja watakaotuma pesa kwenda M-Pesa. Tiketi hizi zitatolewa kwa wateja watakaotuma au kupokea pesa kutoka nchi za Uingereza, Marekani, Jumuiya ya Ulaya (Austria, Ubelgiji, Cyprus, Estonia, Finland, Ufaransa, Ujerumani, Ugiriki, Ireland, Itay, Lithuania, Luxembourg, Malta, Netherlands, Portugal, Slovakia, Slovenia, Spain) katika kipindi cha mwezi Aprili kwa ajili ya Pasaka au Eid.

Kwa nchi za Jumuiya ya Ulaya, NALA inapatikana kwenye App Store na Play Store kwa ajili ya kupakua.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents