HabariSiasa

Polisi walivyojaribu kuiba na kukamatwa Kenya

Chombo kimoja cha habari nchini Kenya kimesambaza picha za video zikonyesha wakati maafisa wanne wa polisi wakidaiwa kujaribu kuwaibia watu wawili shilingi za Kenya milioni 2 ($16,000; £13,000) kwenye barabara moja katika mji mkuu, Nairobi.

Waathirika walikuwa wafanyakazi wa ofisi ya forex na walikuwa wametoa pesa kutoka benki iliyokuwa karibu.

Jaribio hilo la wizi lilizimwa baada ya tahadhari kutolewa. Polisi hao walikamatwa baadaye baada ya wenzao kulinasa gari lao.

Walifikishwa mahakamani Jumanne kujibu mashtaka ya kujaribu kuiba.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents