Nando: I live my life with no regrets (Audio)

Aliyekuwa mwakilishi wa Tanzania kwenye shindano la Big Brother Africa, Ammy Nando amesema hana majuto yoyote aliyonayo baada ya kuondolewa kwenye shindano hilo.

c46a98f0f9e111e2b7ba22000aaa2161_7
Nando akiwa na Dj Fetty wa Clouds FM

Nando ambaye aliondolewa wiki iliyopita kwa kuvunja miongoni mwa sheria za shindano hilo alikuwa akiongea leo kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM.

“I live my life with no regrets,”alisema Nando.

“Sitaki sijui matatizo wala nini, kilichotokea ndio kimetokea, najipanga upya naendelea na maisha mengine. Vingapi vimetokea vingine vizuri nyuma mpaka unapoenda vinakuja vizuri na vizuri kila siku? Tokea nilipotokea mimi nilipokuwa mtoto mdogo nani alikuwa ananijua? Sasa hivi nipo peace yaani, nashukuru kwamba mmenipokea vizuri. Naendelea na maisha, uzuri nimepata platform ya kutengezeza jina langu, kwahiyo naenda hivyo hivyo mpaka huko ntakapofika.”

Msikilize zaidi hapa.

Related Articles

Back to top button