HabariMichezo

Napoli washinda Serie A baada ya miaka 33, mara ya mwisho Maradona alikuwa mchezaji

Wababe wa jiji la Torino Juventus ndio kinara wa kutwa kombe la Serie A mara nyingi akishinda mara 36 na mara ya mwisho ilikuwa msimu 2019-2020.

Mapacha wawili kutoka katika jiji la Milano AC Milan na Inter Milan zote zimeshinda mara 19 na kuwa nyuma ya mabibi kizee wa Torino Juventus.

AC Milan ameshinda mara ya mwisho msimu uliopita 2022/23 na Inter Milan alishinda msimu wa juzi 2021/22.

Genoa mara 9, Torino mara 7, Bologna mara 7, Pro Vercelli ambapo ili Serie C imeshinda mara 7 huku AS Roma akishinda mara 3 na mara ya mwisho ilikuwa 2000/01.

Napoli mabingwa wapya nao wamekuwa sawa na Roma baada ya kufikisha mataji matatu (3) ya Serie A, mara ya kwanza walishinda mwama 1986/87, 1989/90 na 2022/23.

Lazio wana Serie A 2, Fiorentina 2 na Casale 1, Novese 1, Cagliari 1, Verona 1 na mwisho Sampdoria 1.

Juventus walifanikiwa kushinda kombe hili mara 7 mfululizo kuanzia msimu 2014, 2015, 2016, 2017, 2018, 2019, na 2020.

Siku ya jana klabu ya Napoli imefanikiwa kubeba ubingwa baada ya miaka 33.

Mara ya mwisho kuchukua ubingwa Maradona alikuwa mchezaji wa Napoli ingawa kwa sasa Maradona ametangulia mbele ya haki.

Baada ya ubingwa huo ambapo ambapo walitoa sare ya goli 1-1 na klabu ya Udinese kwa hiyo walikuwa nje ya mji wao ambao ni Naples

Jiji hilo la Naples lilipiga mafataki mji mzima kuashiria furaha waliyonayo.

Je klabu ta Yanga siku wakiwa mabingwa maana wapo mbioni kutawazwa mabingwa wanaweza kuiga kitu hiki???

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents