Siasa

Nawapa siku sita tangazeni uchaguzi, msipofanya hivyo narudi mjini na taifa zima- Imran Khan aitikisa serikali 

Waziri mkuu aliyeondolewa madarakani nchini Pakistan Imran Khan hii leo ameipa onyo serikali na kuitaka iandae uchaguzi mpya au ikabiliwe na maandamano makubwa ya umma yasiyokuwa na kikomo.“Nawapa siku sita. Tangazeni uchaguzi ndani ya siku sita. Tangazeni uchaguzi utafanyika mwezi Juni, vunjeni mabunge yote- Ikiwa hatofanya hivyo baada ya siku sita nitarudi tena mjini Islamabad nikiwa na taifa zima ”Imran Khan ametowa onyo hilo baada ya kuwaongoza maelfu ya wafuasi wake katika mji mkuu Islamabad katika maandamano makubwa dhidi ya wapinzani wake wa kisiasa.

Ameonya kwamba wiki ijayo ataitisha tena maandamano ya wafuasi wake nchi nzima ikiwa uchaguzi haukutangazwa.

Hotuba ya kiongozi huyo aliyoitowa leo asubuhi ni kilele cha hali ya vurugu iliyoshuhudiwa ndani ya saa 24 zilizopita katika mji mkuu Islamabad ambako shughuli zilifungwa na kushuhudiwa makabiliano kati ya polisi na waandamanaji nchi nzima.

Serikali ilijaribu kuuzuia msafara kufika katika mji mkuu kwa kufunga barabara zote za kuingia na kutoka Islamabad lakini mahakama kuu nchini humo ilitoa amri ya dharura ya waandamanaji kuruhusiwa.

Related Articles

Back to top button